Forum Navigation

JINSI YA KUPANGA MLO KAMILI

Quote

Kula walau milo 3 iliyo kamili na ususa ( vitafunwa ) walau mara 2 kwa siku pamoja na kunywa maji ya kutosha kuanzia lita 1.5 chagua vyakula kutoka kila kundi katika makundi YAFUATAYO.

Advertise here

 

1. Vyakula vya nafaka, viazi, muhogo na ndizi

         Kwa mfano: mahindi, mtama, mchele, ulezi, ngano, muhogo, ndizi za kupika, viazi vikuu na magimbi.

 

2. Vyakula vya jamii ya kunde na vya asili ya wanyama

        Kwa mfano: maharage, njegere, karanga, mbaazi, kunde, nyama, mayai, maziwa, samaki, dagaa, kuku na wadudu wanaoliwa kama vile senene, kumbikumbi.

 

3. Matunda

        Kwa mfano: embe, ndizi mbivu, papai, pera, chungwa, ubuyu, nanasi, pasheni, parachichi na zambarau.

 

4. Mbogamboga.

       Kwa mfano: mchicha, majani ya maboga, kisamvu, matembele, bamia, karoti, nyanya chungu, nyanya, matango, mlenda, boga na biringanya.

 

5. Mafuta na sukari.

        Kwa mafano: mafuta ya alizeti, nazi, mawese, mbegu zitoazo mafuta, majarini, siagi, sukari na asali.

 

NB: lishe bora hukusaidia kuwa na afya bora, kuzuia upingufu wa damu, kuboresha kuwaji wa kimwili na kiakili hasa kwa watoto. Kuutayarisha mwili kwa ajili ya kunyonyesha.

       

 

error: Content is protected !!